Mpango Husishi wa Watu, Afya na Mazingira katika Bonde la Ziwa Victoria

Mwongozo wa mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wa afya katika jamii

Faster download
Book Thumbnail

Language: sw

Details: © Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, 2014 Hairuhusiwi kuzalisha mwongozo huu wa mafunzo kwa ajili ya shughuli yoyote ya kibiashara. Hata hivyo mwongozo unaweza kunukuliwa kwa lengo la kufundishia, utawala na upangaji wa mipango ili mradi kamisheni ya Bonde la ziwa Victoria (LVBC) itambuliwe rasmi.

Summary: Mwongozo huu wa kufundishia Wataalam wa afya katika jamii (CHWs), timu za afya za vijiji (VHTs), Ushirika wa misitu (CFAs), na wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori unalenga kuwajengea uwezo ili waweze kushirikiana na kaya pamoja na jamii katika harakati zao za kuboresha afya zao na kuhifadhi mazingira katika njia zilizo shirikishi. Kwa kutambua kuwa kaya na jamii zinajihusisha kikamilifu katika kuyaelezea masuala yao ya afya, mafunzo yanalenga kuwawezesha wafanyakazi wa afya katika jamii, timu za afya za vijiji na wafanyakazi wa hifadhi ya mazingira kuweza kusaidia jamii kutathmini hali zao, kutambua mapungufu na kugundua chanzo cha mapungufu hayo ili kuchukua hatua. Kupitia mafunzo haya vikundi vya kijamii vinategemewa kupata ujuzi na stadi zitakazowawezesha kujihusisha moja kwa moja na kaya pamoja na jamii ili kuboresha afya zao, jitihada zao za hifadhi ya mazingira kupitia mijadala yenye heshima na inayothibitika itakayopelekea kuchukua hatua kwa ajili ya kuboresha.