Watanzania Watoa Maoni Yao Kuhusu: Ukuaji wa Uchumi na Upunguzaji wa Umaskini wa Kipato, Hali Yao ya Maisha na Ustawi wa Jamii, na Utawala Bora na Uwajibikaji
Publisher Research on Poverty Alleviation (REPOA)
Ripoti hii inawasilisha matokeo ya utafiti wa Maoni ya Watu kuhusu taarifa za vipengele mbalimbali vya maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na maendeleo yao ya kiuchumi ya hivi karibuni, mabadiliko ya hali zao kimaisha, na ubora na upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi (kama vile upanuzi wa kilimo na ukarabati na utunzaji wa barabara). Utafiti huu pia ulichambua maoni ya watu kuhusu mwelekeo wa shughuli za utawala ikiwa ni pamoja na ushiriki wa wananchi katika masuala ya umma, utungaji sera, na masuala ya rushwa na uaminifu katika jamii.
...