You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Kiswahili - Mazoezi ya Lugha - Mwongozo wa Mwalimu - Darasa la 3
Publisher RTI, Jamhuri ya Kenya, USAID
Published 2018
sw
Pages 180
Download
38.6 MB
Mwongozo huu wa mwalimu wa gredi ya 3 umetayarishwa kwa kurejelea pakubwa mbinu za utafiti iii kumsaidia mwalimu anapofundisha kuwasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wao katika lugha ya Kiswahili. Mwongozo huu umeshughulikia uhusiano na maadili, uhusiano na masuala mutambuko, sehemu nne za ujifunzaji lugha - kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika, vilevile mada zote na maadili yaliyojadiliwa katika mtaala. Mwongozo huu unamwezesha mwalimu kuwapa wanafunzi wa gredi ya 3 mbinu tofauti za kusoma, kujifundisha na kujitathmini na hivyo basi kuakifia malengo lengwa kwa kurejelea sehemu husika za kipindi/somo. Mwongozo huu unarejelea yaliyojiri wakati wa muda wa majaribio ya Tusome. Tusome imedhaminiwa na USAID na kutekelezwa na Wizara ya Elimu. Malengo ya kitabu hiki ni kuwa wanafunzi watakaokamilisha vipindi na masomo kwenye vitabu vya wanafunzi watakuwa wamejikimu na ujuzi wa kuweza kusoma katika gredi ya 3. Pia, wanafunzi wataweza kusoma kwa ufasaha na kuelewa wanachokisoma na kuandika. Hivyo, wanafunzi wakimaliza masomo ya gredi ya 3 watakuwa na uwezo wa kusoma na kujifunza kwa kutumia lug ha ya Kiswahili kama lug ha ya ujifunzaji katika gredi za juu. Yipengele muhimu vilivyopewa kipao mbele kwenye mwongozo huu wa gredi ya 3 ni: Shughuli za ufundishaji ambazo ni za kufurahisha wakati wa kufundisha mada zilizomo kwenye mtaala KICD. Mpangilio maalum wa shughuli za ufundishaji zilizopangwa kwa mtiririko na msambao ufaao kwa kurejelea utafiti uliofanywa katika kufunza na kujifunza Kiswahili. Nakala za kitabu cha mwanafunzi kenye mwongozo huu iii kumwenzesha mwalimu kufanya marejeleo ya moja kwa moja na kwa urahisi anapofundisha. Hadithi tamu zinazolandana na tamaduni na umri wa mwanafunzi zitakazo msaaidia pakubwa katika kukuza ujuzi wake wa kusoma. Maelekezo yaliyopangwa vizuri kumwongoza mwalimu katika kuutumia mwongozo kwa urahisi. Hadithi zilizoandikwa za kiwango cha mwanafunzi na rahisi kusoma ambazo zitamwenzesha mwanafunzi kusoma na kuelewa hadithi husika. Hadithi za mwalimu ambazo zinalenga kukuza msamiati na ujuzi wa kusikiliza wa mwanafunzi. Mwongozo huu umetayarishwa na wataalamu wenye tajriba kubwa kutoka Wizara ya Elimu, Turne ya Huduma ya Walimu, Taasisi ya Masomo Maalumu ya Kenya, na Taasisi ya usimamizi wa Elimu nchini Kenya. Serikali ya Kenya imejitolea kutoa elimu bora kama haki ya kimsingi kwa wanafunzi wote. Azma hii inaambatana na majukumu ya kitaifo na kimataifo yanayohitaji kila nchi kukimu mahitaji ya kielimu na kijamii ya raia wake. Ingawa juhudi zimefonywa kuhakikisha elimu inapatikana kwa urahisi, lengo kuu la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu bora. Serikali ya Kenya imewekeza zaidi katika kuboresha vifoa vya kielimu, miundomsingi pamoja na wafonyakazi iii kuinua kiwango cha elimu inayotolewa katika viwango vyote vya elimu nchini. Mfumo wa elimu unaolengwa umebuniwa kutokana na matokeo ya utafiti wa kina. Kadhalika umejumuisha mbinu zingine zinazokubalika na kutumiwa kimataifo. Msukumo uliopo katika mageuzi ya elimu unatokana na haja ya kuifonya elimu nchini Kenya kuwa kwenye kiwango ya kimataifo na kuwa ya manufaa kiuchumi katika jamii. Serikali inahakikisha kwamba kupitia kwa elimu, wananchi watakuwa wabunifu na kupata stadi za karne ya 21 ukiwemo utafiti, kutatua matatizo, kufikiria kwa kina na kufonya kazi katika hali zote. Vitabu vya TUSOME ambavyo vimeshirikisha maadili ya mtaala mpya vimeandikwa iii kuimarisha uwezo wa kujua kusoma na kuandika, uwezo ambao ni stadi ya kimsingi katika elimu bora. Kitabu hiki kitatumika katika Gredi ya 3 kujifunza na kufundishia Kiswahili katika mtaala mpya. Mpangilio wa kitabu hiki unatilia maanani maantiki na mikakati inayotokana na utafiti iii kukuza stadi za kusoma na kuandika. Vilevile, mpangilio huu utahakikisha kuwa wanafunzi wanapata umilisi ambao ni muhimu kwa viwango vyao. Ninawasihi washikadau wote kuendelea kuunga mkono mageuzi yanayoshughulikiwa katika sekta ya elimu nchini Kenya iii kufikia matokeo bora.
...
Kitabu hiki kinaendana na Kitabu cha Mwanafunzi
...
ISBN: 978 9966 110 03 9
Thank you to RTI, Jamhuri ya Kenya, USAID
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all