You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Elimu ya Mazingira kwa Shule za Msingi - Kiongozi cha Mwalimu
Toleo la Milima ya Tao la Mashariki
Illustrator Athuman Mgumia, Susie Wonfor
Publisher Tanzania Forest Conservation Group
Published 2009
sw
Pages 123

Elimu ya mazingira ni elimu inayowafanya wanafunzi kupata taaluma na ujuzi utakaowasaidia kufahamu na kuenzi mazingira yao, kuishi nayo kwa raha na kuweza kutumia rasilimali zipatikanazo katika mazingira wanayoishi katika njia endelevu na zenye uwiano.

Madhumuni ya Kiongozi hiki ni kuwawezesha walimu wa shule za msingi kufundisha elimu ya mazingira ili vijana katika Milima ya Tao la Mashariki wamalizapo elimu ya msingi wawe na welewa juu ya mambo yanayohusu mazingira yanayogusa misitu na mazingira ya Milima ya Tao la Mashariki. Wanafunzi watakuwa wamewezeshwa kufikiria juu ya matatizo ya kimazingira na pia watakuwa na welewa na stadi za aina tofauti za kuwawezesha kutatua matatizo ya kimazingira watakayokutana nayo katika maisha yao ya baadaye. Hatimaye wataweza kuishi kwa raha pamoja na mazingira yao na wataweza kuelewa namna gani wanaweza kutumia maliasili zao kwa busara katika njia endelevu.

Kiongozi hiki kinazingatia kanuni zilizotajwa katika taratibu juu ya elimu ya mazingira iliyotolewa na Wizara ya Elimu na Utamaduni na kinaunga mkono mabadiliko yanayopendekezwa kuhusu ufundishaji na kujifunza. Kiongozi pia kitatilia mkazo juu ya umuhimu wa mwanafunzi kusoma kwa vitendo katika njia shirikishi pamoja na jamii kuliko kufundishwa darasani pekee.

Taratibu mahususi za Kiongozi ni kama zifuatazo:

Kumhamasisha mwanafunzi aweze kuhusisha anachofundishwa darasani na•

mazingira yake nje ya shule katika jamii.

Kujenga ufahamu wa mwanafunzi kimazingira; uzuri na ugumu wa mazingira, na madhara ya shughuli za kibinadamu katika mazingira.

Kuhakikisha mwanafunzi anaelewa mambo mahususi ya kimazingira katika Misitu ya Milima ya Tao la Mashariki.

Kuwajengea walimu njia bunifu za kufundishia elimu ya mazingira.

Kuwajengea uwezo walimu waweze kufundisha kwa kutumia njia shirikishi. Kutafuta njia za kuziunganisha jamii na shule ili ziweze kufanya kazi pamoja katika kushughulikia matatizo wanayokabiliana nayo wote.

Kuwaleta wanafunzi katika fikira kwamba maliasili zinahitaji kutumika katika njiaendelevu.

Kiongozi hiki kimefuata mtaala wa taifa na kina masomo yaliyotayarishwa kutokana na masomo yaliyopangwa kwa kila mwaka (Darasa la 1-6). Hii inamaanisha kwamba, haitahitajika kazi ya ziada au kupanga darasa nje ya ratiba kutoka kwa walimu- masomo yote yamechukuliwa kutokana na mitaala ya masomo ya Sayansi, Jiografia na Maarifa ya Jamii

...
ISBN: 9987-8958-1-6
Thank you to Tanzania Forest Conservation Group
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all