Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Upandaji wa mimea tofauti tofauti: Mwongozo wa nyanjani
Crop Diversification
Mwaka 2005
sw
Kurasa 73
Pakua 1.3 MB
Kenya ina maeneo mengi tofauti tofauti. Jimbo la kati ni baridi, kule mkoa wa Nyanza kuna mvua nyingi, kuna jangwa kaskazini, na hapa pwani ni joto sana. Kila eneo lina sifa maalum – hali ya hewa, hali ya joto, kiasi cha mvua, na udongo. Kwa sababu hiyo kila eneo lina faida tofauti tofauti shambani. Ustawi wa kilimo hapa Kilifi utategemea uwezo wa wakulima. Ni bora watambue faida na nafasi ya ardhi. Kwa mfano: 1. Mimea gani hufanya vizuri hapa? 2. Wakulima wanaweza kukuza mimea gani hapa kupita maeneo mengine? 3. Mimea gani tunaweza kupanda ambayo wale wa sokoni wanataka kununua? 4. Mimea ipi inastahimili kiangazi? 5. Mimea ipi ina uhitaji wa juu katika soko? Tutaona uwezekano mkubwa wa shamba wakati zile taratibu za kulima zinatumia kikamilifu sifa ya ardhi yake. Hili wazo ni msingi ya Upandaji wa Mimea Tofauti Tofauti (Crop Diversification).
...
Shukrani kwa Sokoine National Agricultural Library
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.