You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Mwongozo wa Walimu kwa Kitabu Cha Uamuzi Wa Afya
Published 2017
sw
Pages 95
Download
0.8 MB
Mradi huu unasaidia watu kufanya uamuzi bora zaidi kwa afya yao kwa kufikiria kwa makini kuhusu matibabu. Mpe mtu samaki na watakuwa na samaki kwa siku hiyo. Mfunze huyo mtu kuvua samakina atakuwa na samaki maisha yake yote. Huu ni msemo unaojulikana vizuri sana. Cha maana ni afadhali kumfunza mtu kufanya kitu mwenyewe kuliko kuwafanyia tu. Kuna miradi mingi inayowaeleza watu uchaguzi wa kufanya kuhusu matibabu. Miradi hii huwapa watu majibu. Mradi wa Uchaguzi wa Ufahamu wa Utunzaji wa Afya (IHC) unahusu vile mtu yeyote anaweza kujifanyia uchaguzi mwenyewe kwa kufikiria kwa makini. Kufikiria kwa makini kuhusu matibabu inahitaji kuuliza maswali. Kiini cha mradi huu ni maswali gani yanayofaa kuulizwa na kwa nini yaulizwe. Mara nyingi watu wakitaja “matibabu”,huwa wana maana ya kumeza dawa. Hata hivyo, katika mradi huu, “matibabu” ni chochote ufanyacho ili afya yako ibaki nzuri au izidi kuwa bora. Kwa hivyo, kumeza dawa,kupasuliwa, kutumia vifaa vya tiba, kufanya mazoezi,kula au kunywa kitu,na kuepukana na kitu yote ni matibabu. Kuna aina tatu ya maswali unayofaa kuuliza kuhusu matibabu: • Maswali kuhusu madai ya matibabu • Maswali kuhusu kulinganisha matibabu • Maswali kuhusu uchaguzi wa utunzaji wa afya
...
Kitabu hiki ni mwongozo wa Mwalimu unaoendana na kitabu cha: Kitabu cha Uamuzi wa Afya: Kujifunza kufikiria kwa makini kuhusu matibabu
...
Translated by
Suzanne Z. Koteng' Nyamory, Steven Ochieng, Margaret Kaseje
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all