Publisher Tanzania Publishing House
Wazazi wengi siku hizi wana mwamko mkubwa sana wa kuwapeleka watoto wao kwa matibabu hospitalini na vituo vya afya. Matokeo ni kwamba, kama mama akimpeleka mtoto kwenye kituo cha afya au hospitali kwa matibabu madogo au kutaka ushauri juu ya afya ya Mtoto, inamchukua muda mwingi sana kupata huduma kwa sababu ya wingi wa wanaohitaji huduma na uchache wa vafanyakazi. Tatizo hili mara ingine linawafanya baadhi ya mama kuchukua njia ya mkato na kwenda kwenye hospitali za biaafsi na kulipa pesa nyingi sana kwa huduma au kwenda kutafuta dawa za mizizi kwa waganga wa kienyeji.
Madhumuni ya makala hii si kufanya watu wote wawe madaktari bali ni kuwasaidia wazazi ii wajisaidie wenyewe na wawasaidie, watoto wao kwa mambo madogomadogo yanayohusu magonjwa ya watoto wadogo. Matatizo mengi ya afya au magonjwa ya watoto wadogo, yangeweza kutatuliwa mapema na vizuri zaidi nyumbani, Ni vizuri kuwapatia watu, wengine katika jamii yetu, baadhi ya utaalamu tulionao badala ya kuuhodhi kama wanavyofanya mabepari. ili watoto wadogo wapate afya. njema na vifo vipungue kutokana na maradhi, inatubidi tuwahusishe wazazi katika kutunza afya ya watoto wao badala ya sisi kuwatunzia watoto wao hasa katika matatizo na magonjwa madogo madogo. Kuna tumaini kuwa, wazazi baada ya kusoma habari hizi juu ya utunzaji wa watoto katika afya njema na magonjwa, wataweza kutoa huduma za kwanza kwa watoto wao kabla ya kuwapeleka kwa waganga ambao m haba nchini. Pamoja na hayo, wazazi lazima wachukue tahadhari. ya kutochelewa kuwapeleka watoto wagonjwa hospitali kwa sababu walikuwa wanajaribu, kwa muda mrefu kuwatibu watoto hao majumbani kama kwamba wao ni madaktari. Kwa wazazi, utaalamu kidogo, unawafaa tu kutoa huduma ya kwanza kwa watoto wagonjwa kwa upesi hali huku wanajitayarisha kuwapeleka watoto hospitali ikiwa magonjwa yao ni makali.
Vilivile inatumainiwa kwa watoto wa shule wakisoma kitabu hiki wataweza kusaidia sana mama zao kutoa huduma za kwanza za dharura kwa wadogo zao wakiwa wameugua ghafia huko majumbani. Ili kueneza yaliyomo ndani humu vijijini, inafaa watoto wengi wa shule wasome kijitabu hiki na kwani mara nyingi wao ndio wanaojua kusoma majumbani kwao.
...