"Umezaliwa wa Kiume, Dhihirisha Uanaume"
Dunia ya leo ina WANAUME wachache sana pamoja na kuwa na maelfu ya watu wa jinsia ya kiume. Ni wazi kwamba unaweza kuwa mtu mzima wa kiume lakini bado usiwe MWANAUME. Unaweza kuonekana mtu mzima wa kiume lakini ndani yako Wewe ni MVULANA. Hii ni kwa sababu UANAUME sio jinsia bali MAJUKUMU. Unaweza kabisa kuzaliwa wa kiume, lakini kuwa MWANAUME ni mchakato. Zipo hatua, malezi na mafunzo mbalimbali ya kujitambua na kutekeleza ili ufanyike MWANAUME kweli kweli.
...