Swali: Je, umejifunza zaidi kutoka kwa wazazi wako ama kupitia uzoefu wako ulimwenguni?
Methali hii hutumika wakati mtu amekosa na kupata madhara, haswa kama ameonywa... kama vile dereva wa lori katika picha hii (kutoka Oxfordshire, Uingereza). Bila kujali kama ulifunzwa na wazazi, hatimaye lazima ukabiliane na ukweli wa maisha halisi. Ona pia: Mtoto akilia wembe, mpe
Kuna shairi lililotungwa na Akilimali Snow-White juu ya methali hii:
ASOFUNZWA NA WAZAZI, HUFUNZWA NA ULIMWENGU
na Akilimali Snow-White
Zama walinipumbaza, wazee kwa kunilea,
Nikashindwa kujifunza, myendo mipya ya dunia,
Leo najipendekeza, kwa walimwengu sikia,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.
Kazi zote singeweza, bila kuwanyenyekea,
Kutii kuwembeleza, kisha kuwatumikia,
Hata nikawapendeza, wakanifunza kwa nia,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.
Sasa kusema naweza, Kizungu bila udhia,
Kama vile Kingereza, na lugha zingine pia,
Kwa juhudi najifunza, hata zimenielea,
Asofunzwa na wazazi,...
Read more...