You need to login to view profiles OR to update your profile

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
New announcements
Discussions
Proverbs

Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa

Join
or login
to VOTE for Proverb of the Month
Votes
0
Updated 5mo ago
by
View this proverb in English
Better late than never
Siku moja, mfanyabiashara mashuhuri alitafuta msaidizi. Alipokea maombi na CV za watu wengi sana, lakini wawili tu walikidhi vigezo: Amina na Baraka. Ili kuamua kati yao, aliwaita wote wawili, na akawaalika waje kwaajili ya mahojiano ya ajira, kesho yake asubuhi. "Saa tatu kamili -- vaa mavazi ya kazi, na usichelewe!" Akawaonya.

Kesho yake Ali aliwahi kuamka, akavaa suti yake nzuri, na alipanda basi kijijini kwake saa 2. "Bora kinga kuliko tiba" alifikiria. Njiani kuelekea mjini, basi ilianza kutoa moshi. Abira wote walishuka na waliachwa porini. Hapo hapo mvua ilianza kunyesha. Kila basi lililompita, Ali akaomba nafasi, lakini, kutokana na hali ya hewa, mabasi yote yalikuwa yameshajaa. Kwa hivyo ikabidi atembee kwa miguu. Ilipotimia saa tatu, bado Ali alikuwa mbali na mji, na mvua ikawa kali zaidi na zaidi. "Lazima niendelee" akajiambia, "Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa."

Wakati huohuo mjini, Baraka aliamka ghorofani kwake, na akashtuka ghafla akiona jua lilikuwa limeshafika mbali angani. "Aisee! Niliweka alarm! Simu yangu ina shida gani sasa?" Alitazama saa ukutani: Saa tatu kamili. "Bora niache tu. Hata nikiondoka saivi, bado nitachelewa kufika. Si alisema usichelewe? Hatamwajiri aliyechelewa." Kwa hivyo Baraka, akiwa na huzuni, akalala tena.

Saa nne na nusu, hatimaye, Ali alifika ofisini kwa mfanyabiashara na kugonga mlango, suti yake ikichuruzika maji na matope sakafuni. Mfanyabiashara akajibu. "Si nilikwambia vaa mavazi yanayofaa na usichelewe? Sasa umechelewa zaidi ya saa limoja na mavazi yako yamechafuka. Niambie nitawezaje kukuajiri baada ya hapo?" Kisha Ali akaeleza yote yaliyomtokea. Mfanyabishara akamjibu "Nimejifunza mengi kuhusu wewe kutoka kwa hadithi yako Ali. Ukiwa na kusudi kichwani, utafanya kazi kwa bidii, na pale unapokutana na vikwazo hukati tamaa, hata kama umechelewa. Nakwambia, wewe ndiye wa kwanza kufika leo. Mwingine alikosa kabisa. Nitakuajiri wewe."

Mafanikio makubwa huanza na makosa mengi, lakini baada ya muda, uvumilivu na ustahilimilu huleta matunda. Kukosa ni uanadamu, lakini Mungu ni mvumilivu sana kwetu. Anatupa nafasi nyingi za kujifunza na kujaribu tena, ilimradi tusikate tamaa.

Wengine wanasema methali ya "Better late than never never" inatoka kwa kitabu cha The Canterbury Tales, kilichoandikwa na Chaucer miaka ya 1390.
Better than never is late
“Bora kuliko kamwe ni kuchelewa
-The Canterbury Tales, The Canon's Yeoman's Tale
Wengine wanasema chimbuko la kweli ni kitabu cha Historia ya Roma, kilichoandikwa na Livy takriban mwaka wa 20 KK.
Lilatini: potiusque sero quam numquam
Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa
- History of Rome, Book 4

Methali ya Kiingereza inayoendana ni:
It's never too late
Hakuna kuchelewa
 Methali ya Kiingereza inayopinga:
Don't close the gate after the horse has bolted.
Usifunge mlango baada ya farasi kukimbia

Methali ya Kihindi: 
जब जाति तब सवेरे
Wakati wowote unapoamka, ndo asubuhi yako

Details Fikiria kama umechelewa Mahojiano ya Ajira. Ungefanyaje? Next time unapofikiri "Nimeshachelewa" jiambie "Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa." Kwa mfano makala hii ya Methali ya Siku ilichelewa, lakini sasa unaisoma - Asante!
Sources
The Canterbury Tales, The Canon's Yeoman's Tale
History of Rome, Book 4

Better late than never (Wiktionary)
Close the stable door after the horse has bolted (Wiktionary
Loading...
Loading...
Login to view and post comments
Methali yetu ya leo inasemwa pia kama:
Mtaka cha mvunguni sharti ainame
Methali hii hutumika kuwahimiza watu kufanya kazi kwa bidii na kujitahidi. Hatupaswi kutarajia kupata vitu tunavyotafuta isipokuwa tumekubali kuvitafuta katika mahali ambapo ni vigumu kupafikia.

Hapa kuna hadithi fupi inayoeleza methali hii, juu ya Mulla Nasreddin, mhusika mcheshi katika ngano za Kisufi.
Mulla [Nasreddin] alikuwa amepoteza pete yake sebuleni. Aliitafuta kwa muda, lakini kwa kuwa hakuipata, alitoka nje hadi uani na kuanza kuchungulia pale. Mkewe, ambaye aliona alichokifanya, akamwuliza: “Mulla, umepoteza pete yako sebuleni , kwa nini unaitafuta uani?” Mulla alishika ndevu zake akisema: “Chumbani kuna giza na sioni vizuri. Nilitoka nje kwenda uani ili kutafuta pete yangu kwa sababu kuna mwanga mwingi zaidi hapa.
- Usimulizi wa Houman Farzad. Imetafsiriwa kwa Kiingereza kutoka lugha ya Kiajemi na Diane L. Wilcox (1989), halafu nimeitafsiri kwa Kiswahili.

Kwa Kiingereza, kuna hadithi inayosimuliwa juu ya mlevi anayetafuta pesa (au funguo) karibu na taa. Hili ni toleo liliochapishwa katika gazeti ya Boston Herald (mwaka wa 1924): 
[Afisa wa polisi alikutana na mwanamume akipapasa-papasa akipiga magoti] “Nilipoteza noti ya $2 kwenye barabara ya Atlantic,” kasema mwanamume huyo. "Nini kile?" aliuliza afisa aliyeshangaa. "Umepoteza notiya $2 kwenye barabara ya Atlantic? Kwa nini basi unaitafuta hapa Copley Square?" “Kwa sababu,” akasema akiendelea na utafutaji wake, “mwanga ni bora hapa."

Hadithi hii imekuja kujulikana kama "Streetlight effect" katika sayansi.

Asante kwa mshiriki mwenzetu kwa kupendekeza methali hii! Je, una methali ya kupendekeza? Shiriki hapa!
...

Mchoro huu umetengenezwa kwa kutumia Akili Bandia (AI). Unafikiriaje?

Updated 5mo ago
by
Many people are afraid to ask questions because they don't want to be seen as stupid. But asking questions is the best way to learn from others.

Asking questions also helps others around you. Have you ever hesitated to ask a question because you thought others already understood... but later you realized they didn't either? 

This proverb is similar to the English saying, “There's no such thing as a stupid question.”
...
Updated 5mo ago
by
Kila kazi kubwa katika maisha huhitaji kufanyika kwa hatua ndogo, siku baada ya siku. 

Je, unajua methali zingine zinazofanana na hii au zinazotoa dhana hiyohiyo? 

Msemo huu unakumbusha shairi liitwalo "Vitu Vidogo" na Julia Abigail Fletcher Carney: 
Matone madogo ya maji,
Chembe kidogo za mchanga, 
hutengeneza bahari kubwa
Na ardhi ya kupendeza

Vivyo hivyo zile dakika ndogo,
ingawa ni ndogo,
hutengeneza enzi za milele. 
Julia Carney alitunga shairi hili mwaka wa 1845 darasani akiwa mwanafunzi darasani -- na alipewa dakika 10 tu kuliandika!
...
Updated 5mo ago
by
Methali hii inatoka Kiingereza "A penny saved is a penny earned." Maana yake, mia inayobaki mfukoni inaweza kutumiwa kwajali ya madhumuni mengine. Mifano: Inaweza kutumika kwaajili ya kununua kitu kingine, unaweza kukopesha au kuwekeza ili kuingiza riba au pesa zaidi katika siku zijazo. Katika uchumi, kanuni hii inaitwa Opportunity Costs (gharama za kukosa fursa). Tunapotumia pesa au muda kwa jambo limoja, tunapoteza pia fursa ya kuzitumia kwajili ya jambo lingine.

Methali hii huhusishwa na Benjamin Franklin, lakini si chimbuko halisi, wala hakuandika msemo huu kamili. Misemo karibu na huu ilichapishwa kabla yake. Kwa mfano: 

A penny spar'd is twice got.
Senti iliyookolewa hupatikana mara mbili.
- Outlandish Proverbs by George Herbert (1640)  
 
Katika Poor Richard's Almanac (1736), Benjamin Franklin alinukuu methali hii na alifafanua vizuri kanuni ya Opportuinty Cost hivi:

Vidokezo kwa Wale Wanaotaka kuwa Matajiri

Matumizi ya pesa ndiyo faida zote zinayopatikana ukiwa na pesa.
Kwa pound [£] sita kwa mwaka [yaani riba] unaweza kutumia  £ mia [yaani kupitia mkopo], kama unajulikana kama mwaminifu na mwenye busara.
Anayetumia groat [senti 4] kwa siku bure, hutumia pound £ zaidi ya sita kwa mwaka, ambazo ni bei ya kujipatia matumizi ya pound £ mia moja.
[Kwa hivyo] Anayepoteza muda wake wa thamani ya groat [senti 4] kwa siku, siku moja na nyingine, anapoteza fursa ya kutumia pound mia moja kila siku.
Anayepoteza muda wa shilingi tano kwa uvivu hupoteza shilingi tano, ni kama amezitupa tu baharini.
Anayepoteza shilingi tano sio tu kwamba anapoteza kiasi hicho, bali anapoteza pia faida yote ambayo ingeweza kupatikana kwa kuzitumia katika shughuli zake, ambayo, akiwa kijana, wakati wa uzee ingefikia kiasi kikubwa cha fedha.
Tena: anayeuza kwa mkopo huongeza bei ya kile anachokiuza kwa kiasi sawa riba angaliingiza na pesa hizo kwa kipindi ambacho atazikosa. Kwa hivyo, anayenunua kwa mkopo hulipa riba kwa kile anachonunua, na anayelipa pesa mara moja kwa kila anachonunua hukoa fursa ya kuzikopesha kwa wengine, kwa hivyo aliye na kitu alichonunua ameshalipa riba kwa matumizi yake.
Hata hivyo nasema kulipa mara moja unaponunua ni bora, kwa sababu anayeuza kwa mkopo anatarajia kupoteza asilimia tano ya mikopo; kwa hivyo anaongeza bei ya kile anachokiuza kwa asilimia ileile ili kuzuia hasara. Wanaolipa kwa mikopo hulipa kodi mara moja. Anayelipa kwa pesa mara moja anaweza kuzuia kodi hii
"Senti iliyohifadhiwa ni senti mbili hakika;
[haba] kwa siku ni [nne] kwa mwaka."
 
Basi, unapofikiria kutumia muda au pesa zako katika jamblo fulani, jiulize, ningekosa, ningepata fursa zipi? Pesa hizi zingeweza kutumikia vipi? Mifano: kumkopesha mwingine, kurudisha madeni uliyonayo, kubuni kitu kipya au kuwekeza katika kitu ambacho kinaweza kuleta faida kubwa mbeleni.
...
Updated 5mo ago
by