Kimeandikwa na
Mchapishaji Feed the Minds
Usimulizi wa hadithi una nafasi muhimu katika jamii ya Afrika, hasa katika familia. Kitamaduni, watoto kujifunza kuhusu mila, dini na utamaduni wanaposikiliza hadithi kutoka kwa wazazi wao. Hadithi huwasaidia watu kuelewa dunia na watu wengine. Hata hivyo, baadhi ya hadithi kuhamasisha ukabila, na hadithi zinaweza kutumika kutekeleza dhuluma na mashinikizo. Hivyo basi, uteuzi makini ni muhimu. Hadithi miongoni mwa watu wazima mara nyingi hutumika kwa kuburudisha, bali pia zinaweza kuwa chombo cha nguvu cha kujenga amani katika familia na jamii
zilizogawanyika. Hadithi hutoa fursa ya kutatua migogoro na kusaidia watu kusamehe na kupatanishwa. Usimulizi wa hadithi unaweza kuwa wa thamani katika kuwafariji wanao omboleza msiba au hasara zozote. Msimulizi wa hadithi anaweza kunufaika kwa kuhisi kuwa hayuko ‘peke yake’ na ya kwamba kuna watu ‘waliosikiliza’ masaibu yake. Anayesimuliwa anaweza kusikia na kuelewa matukio kupitia kwa macho na masikio ya mtu mwingine. Hatua za usumulizi wa hadithi zikiwezeshwa kiustadi, zinaweza kusaidia jamii kuandaa mipango ya uponyaji na maendeleo.
Sanaa ya usimulizi wa hadithi imekuwa ikipotea katika baadhi ya jamii kwa njia ya vita na migogoro, kutokana na kuvunjika kwa familia au kuongeza kwa teknolojia....
...