You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Maswali Yaulizwayo na Jamii kuhusu Afya ya Akili na Majibu Yake
Publisher Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth, Jamana Printers Ltd
Published 2020
sw
Pages 36
Maana ya Afya ya Akili inahusu ustawi wa mtu katika ngazi kuu tatu: nafsi na utashi, akili na fikra, mwili na hisia/mihemuko. Afya ya Akili inahusiana sana na jinsi mtu anavyofikiri, anavyojisikia na anavyotenda.. Mtu akifikiri vizuri ni rahisi kujisikia vizuri na kutenda mambo mazuri. Mtu akiwa na fikra hasi, atajenga hisia hasi na kisha matendo yake yatakuwa hasi pia. Kwa hiyo Afya ya Akili ni ile ambayo inamwezesha mtu kujitambua kuhusu uwezo, vipaji na hata udhaifu wake, anachopenda na asichopenda, anaweza kudhibiti na kuhimili changamoto za kawaida za kimaisha, anaweza kufanya shughuli zake za kimaisha na kuchangia katika familia na jamii.
Matatizo ya afya na ugonjwa wa akili hayabagui wala hayachagui, ni kama magonjwa mengine yanayoweza kumkuta mtu yeyote, wa
jinsia zote, rika, desturi, rangi na dini zote, walio na wasio na elimu, matajiri na maskini, walemavu na wasio walemavu. Matatizo ya afya na ugonjwa wa akili hayatokani na udhaifu wa mtu au tatizo katika hali ya mtu. Watu wanapozingatia tiba huweza kuudhibiti ugonjwa wa akili na kurejea kwenye hali zao za kawaida. Kuwajali na kuwatunza, watu wenye ugonjwa wa akili katika jamii zetu ni ulinzi muhimu sana unaowasaidia kurejea kwenye maisha yao ya kawaida.
Jamii nyingi za kiafrika huwatenga na kuwaficha watu wenye
ugonjwa wa akili kama vile kuwafungia kwenye chumba ambacho wakati mwingine huwa kina giza hivyo kuwazidishia athari zaidi kiakili.
Jamii nyingi huwapa majina yasiyofaa watu wenye dalili za ugonjwa wa akili, majina kama vile: kichaa, chizi, dishi limeyumba, mwehu, mwendawazimu, mtambo, chupa imepooza n.k. Zipo familia ambazo kwa kuhofia kunyanyapaliwa na jamii, huwaficha watu wenye ugonjwa wa akili au kutokuwa wazi kusema ndugu yao ana ugonjwa wa akili.
Hili linaweza kutokea kutokana na hali ya kujilinda dhidi ya dhana potofu ya kwamba familia hiyo ina laana, mkosi, mapepo au mizimu mibaya hususani wakati wa kuchumbiana. Hali hii huathiri watoto, vijana, wazazi, wenza, marafiki na jamii kwa jumla.
Kuongozeka kwa matatizo ya afya ya akili ni changamoto kwa
maendeleo ya jamii yote hivyo ni muhimu sana kwa jamii kuchukua hatua stahiki katika kuhamasisha uthabiti wa afya ya akili na upatikanaji wa matibabu ya magonjwa ya akili. Ni kutokana na ongezeko hili shirika lisilo la kiserikali TEWWY limeamua kuchukua hatua ya awali ya kuandaa kitabu hiki chenye maswali na majibu kuhusu afya na baadhi ya magonjwa ya akili kwa ajili ya kuelimisha na kuhamasisha jamii kuchukua hatua japo kwa kuanzisha mazungumzo juu ya afya na magonjwa ya akili.
Maswali yaliyomo kwenye kitabu hiki yalikusanywa kutoka kwa vijana na watu wazima. TEWWY kwa kushirikiana na jopo la wataalamu wa afya ya akili, sayansi ya jamii, sanaa na elimu waliyapitia maswali hayo na kuandaa majibu. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha rahisi ili kuleta uelewa na ufahamu kwa msomaji.
...
Kitabu hiki kimetayarishwa na asasi ya TEWWY kwa hisani ya HIVOS ya Uholanzi katika mradi wa VOICE kwa kushirikiana na wataalamu kutoka sekta ya afya, maendeleo ya jamii, elimu na sanaa. Vijana na kina mama watu wazima walishiriki kuibua maswali haya ndani ya jamii.
...
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all